Friday, December 3, 2010

UKAME MKALI WAJA TANZANIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 10


WATANZANIA WAMEMWACHA MUNGU, WAMEELEKEA MIUNGU YA DUNIA HII.

Kama BWANA MUNGU wa Islael, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua katika Nchi hii kwa kipindi cha miaka kumi (10), ila kwa neno langu.

Bwana wa majeshi aliyezifanya mbingu na nchi kwa uweza wake mkuu na kwa mkono wake ulionyooshwa amegadhibika kwa sababu ya watu kuabudu miungu ingawa wanadai wanamjua Mungu (WAMEOKOKA) na mbaya zaidi wengine wanajiita ni watumishi wa mungu na mitume na manabii lakini kumbe ni waongo, na watu wengi wamewakimbilia watushi hao ili kutafuta mahitaji yao na si kumtafuta Mungu aliye hai. Watu wamekwenda kwa waganga wa kienyeji na wachawi kutafuta msaada badala ya kwenda kwa BWANA wa Majeshi aliyezifanya Mbingu na Nchi (wamekwenda kwa Ashuru) Hosea 5: 8-14.

Ingawa watu wanasema wanampenda BWANA, lakini ni wanafiki kabisa, ni:- Washerati, wachafu, mafisadi, waabudu sanamu, wachawi, wana uadui, wagomvi, wana wivu, wana hasira, ni watu wa fitina, ni watu wa faraka, wazushi, wanahusuda, walevi, walafi, na mambo mengi yanayofanana na hayo.

Bwana amegadhibishwa nayo, wamesikia habari za MUNGU wa kweli, lakini hawataki kumwabudu yeye. Hivyo waTanzania watashuhudia Dhiki ya Njaa kali sana ambayo haijawahi kutokea katika taifa hili. Labda katika taabu yao watatubu! Hosea 5:15.

Mungu amelijilia taifa la Tanzania kwa ghadhabu labda litatubu, na lisipotubu litaangamia.

SAMSON MLATA KUINULIWA
Mawasiliano:
+255 765 274587
+255 658 274587

No comments:

Post a Comment