Friday, December 3, 2010

SABABU 7 ZILIZOPELEKEA MAJIMBO YA NYAMAGANA & ILEMELA JIJINI MWANZA KWENDA CHADEMA KTK NGAZI YA UBUNGE NA MADIWANI.

Na: Mwandishi wetu.
Inafahamika wazi katika jimbo la Nyamagana kuwa kiongozi wa siasa hasa Mbunge kukaa madarakani zaidi ya miaka mitano ni kazi sawa na Mende kuangusha kabati au sisimizi kumeza chungwa.

Kipindi hiki matokeo yametisha sana kwa majimbo yote ya jiji la Mwanza, tumeshuhudia Magu mjini watu wakipigwa mabomu ya machozi hasa wale waliokuwa wameamua kukaa umbali wa mita 200 kusubiria hadi kieleweke, yaani kusiwepo na uchakachuzi wa kura. Vivyo hivyo mwanza mjini hasa jimbo la Nyamagana ambapo watu waliamua kuka umbali wa mita 300 na kusubiri hadi kieleweke. Chamsingi tu ifahamike wzi kuwa watu wakisema hapana na kweli huwa ni hapana, na kumwongoza binadamu ni kazi kubwa sana ambayo ni bora upewe Ng’ombe kuchunga maana utawapeleka utakako hata kwa fimbo.

Baadhi ya hisia zangu kuhusu chama cha mapiduzi (CCM) kushindwa kwa kishindo katika majimbo ya Ilemela na Nyamagana ni kama zifuatazo.

i. Watu wametapeliwa pakubwa sana na wafanya bishara ya upatu yaani DECI. Hivyo watu nadhani wamekaa na kufikiria kuwa hawa watu walikuwa na vibari kutoka seriaklini sasa je, iweje waendeshe biashara haramu namna hii bila uongozi kulitambua hilo na ukizingatia wadhili wa mambo ya ndani anaishi eneo hilihili na pia ofisi za DECI zilikuwa karibu mno na ofisi za TRA je, serikali haina vyanzo vya habari vinavyofanya kazi kwa wakati mwafaka au? tatizo liko wapi. Je, wabunge waliowapatia dhaman ya kuwasemea Bungeni walilichukuliaje hilo tatizo? Kwahiy basi kutokuonyesha mchango chanya wabunge wao kwa wananchi katika matatizo yaliyowakabili hasa DECI kumefanya wabunge hawa wamwagwe chini kuonyesha fundisho.
ii. Shirika jingine ambalo hadi sasa wanamwanza wanaliona ni la wizi ni People’s Unity for Development in Africa (PUFDIA). Wengi wametapeliwa pesan nyingi sana na mbaya zaidi walioibiwa ni wale maskini wa kutupwa, wamepewa ahadi feki, siku zimeenda hakuna matekelezo na ofisi zimefungwa hakuna hata mtu anayeonekana kuifungua hiyo ofisi. Zoezi la kukusanya pesa kutoka kwa wananchi masikini lilifanyika katikati ya jiji la Mwanza na Dar es salaam, lakini hadi sasa hakuna aliyeona mtu akinufaika na PUFDIA hivyo watu wakaamua kuinyima CCM kura katika majimbo ya Ilelema na Nyamagan.
iii. Usaliti kutoka ndani ya CCM. Inawezekana kabisa kuwa ushindi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Ilemela ukawa umesababishwa na Mbunge wa CCM jimbo la Nyamagana na pasipokujua au kwa kudhamilia kabisa mbunge wa CCM jimbo la Ilemela kukisaidia pia chama cha CHADEMA kumngo’a mbunge wa Nyamagana CCM. Haikuwa rahisi kwa mbunge wa Ilemela kuondoka madarkani kiurahisi hivi, ila tunamshukuru sana kaonyesha ukomavu wa kisiasa kwamaana alisaini mapema sana na watu hawkumwaga damu kwa kudai haki yao. Pia haijapata kutokea hapa nchini waziri wa mambo ya ndani kushindwa kwa urahisi namna hii.
iv. Machinga na mama ntilie wa jiji la mwanza wamechoshwa na wagambo kuwatimua katika maeneo yao ya kazi, awamu hii walikuwa wameamua kujiandikisha kwa wingi na kusimamia kwa asilimia zote, waliamua kuzuia njia ili yasiingie wala kutoka magari katika eneo lakujumlishia kura ili hadi kieleweke. Na kweli kilieleweka japo watu walifukuzwa sana kwa mabomu ya machozi, walichoma matairi barabarani ili hai yao ipatikane. Na mara baada ya kutangaziwa matokeo yao fujo zikatulia kabia, kumbe inapotokea njia zote za kuelekea kwenye haki zinapokuwa zimefungwa, machafuko huwa hayakwepeki. Mwanza pasingekuwa kama palivyo sasa endapo matokeo ya uchaguzi yangechakachuliwa, kwa sababu dalili zilikuwa zimeanza kuonekana mapema sana hasa kwa barabara kufungwa na raia na kuruhusu magari ya askari tu na maji ya kuwaha kupita huku wakiimba “gari letu eeh, gari letu eeh”.
v. Wananchi wamechoshwa na chama tawala, inawezekana kabisa kuwa miaka iliyopita walidanganywa kwa ahadi walizopewa hivyo wameamua kuonyesha kuwa mwaka 2010 hawadanganyiki.
vi. Aliyekuwa mgombea ubunge ambaye sasa ni Mbunge wa CHADEMA jimbo la Nyamagana Mheshimiwa WENJE kuwekewa pingamizi kuwa siyo raia wa Tanzania alijizolea umaarufu kwa watu zaidi ya mbunge wa kigoma kaskazini bwana Zitto Kabwe (CHADEMA) kipindi alifukuzwa bungeni kwa kuibua hoja nzito za ufisadi. Wananchi hasa wapiga kura wa Nyamagana waliamua kufanya mbaya dhidi ya bwana L. Masha kwa mantiki ya kuwa anatumia madaraka vibaya.
vii. Kitabu cha “Mafisadi wa Elimu” kilichoandikwa na Bwana Msemakweli kilimshushia heshima aliyekuwa mbunge wa Ilemela. Sijasema kweli yeye ni fisadi wa elimu ila naonyesha kuwa wananchi walizinduka usingizini na kuanza kufuatilia nyenendo zake kwa ukaribu zaidi.

Naomba kuishia hapa, maana hapo ndipo mwisho wa uoni wangu kuhusiana na siasa. Na mtu yeyote asije kuninukuu popote kwa sababu hizi na hisia tu “hypothesis” hazina utafiti wa kutosha. Shukrani zimwendee aliyeachia madaraka jimbo la Ilemela maana aliwahi kusaini bila bugudha yoyote ile na kwakuwa ni mjasiliamali mzuri sana basi Mwenyezi Mungu atamsaidia kukaa chini aone kakosea wapi na mara nyingine afaulu zaidi ya sasa ambapo kura hazikutosha.

Shukrani ziwaendee maaskari wote jiji la Mwanza, maana walionyesha ujasiri mkubwa sana wakati wa uchaguzi katika kuwatuliza wananchi wasifanye fujo, tena walifanikisha hilo kwa asilimia kubwa sana bila watu kumwaga damu.

Mwisho liwe fundisho kwa wote wenye nia ya kuongoza wananchi maana hata ninyi mliokamata nafasi hizo sasa hivi uchaguzi ijao mnaweza kung’atuliwa kwa ulaini sana endapo mtabolonga bungeni. Hatujawatuma mkasinzie mjengoni, tumetuma wawakilishi wenye kutoa hoja kwa mujibu wa sheria na vifungu, wenyekuvumilia vitisho kutoka vyama pinzani na kuongea vitu mlovifanyia utafiti wa kutosha huku mkikumbuka kuwa mnaongoza wananchi waliokaliwa na mataifa ya kibepari yaliyorudi tena kwa gia ya uwekezaji “full exploitation”. Piganieni kuibadili katiba ya nchi, na kutengua mikataba mibovu na kuchunguza makampuni yanayobadili majina kama CELTEL-ZAIN-AIRTEL TZ. Chunguzeni kuna ukweli wowote hapo au ni wizi mtupu, kupitia ukwepaji kodi serikalini. Mungu ibariki Tanzania.

+255 783 700083

No comments:

Post a Comment