Saturday, December 4, 2010

TUAMKENI SASA KUMEKUCHA, MWANAMKE HANA NAFASI YA KUTUTAWALA.

Mwanamke yeyote aishie hapa duniani ni kiumbe dhaifu sana, akiliyake haipishani nay a motto mdogo. Ndiyo maana hata serikali za nchi nyingi zimeweka widhara ya wanawake na watoto kwa kumlinganisha mwanamke na watoto wadogo. Chakushangaza sasa hivi nchi zenye mbilikimo wa siasa na wenye mipango lukuki ya kupokonya hela za kodi za wananchi zimeamua kuwapa nafasi wanawake nyazifa za juu sana serikalini bila kuona kuwa ni hatari sana kwa taifa.

Kwaufupi ni kwamba, mwanmke ni kiube ambaye hafai kabisa hata kidogo kuendesha huduma za jamii, mfano mzuri ni wa Bwana YESU wakati anachagua mitume wake 12 hakuthubut kumchagua mwanamke kwa sababu aliona kuwa kutakuwepo na matatizo ya rushwa, tamaa a ngono, wivu, ufuska, ufisadi, na kadhalika. Hii inatukumbusha tu kuwa tumesahau tulikotoka hivyo tunahribu tunakokwenda.

Kitu kingine cha kuzingatia hapa ni Mateso aliyoyapata Samsoni yalitokana na usaliti wa mkewe ajulikanye kwa jina la Delila. Haiwezekani hata kidogo kumweka mwanamke mbele kusimamia chombo cha umma.

Kifo cha Rwanda Magere “the rock” kilisababishwa na mwanamke ambaye alijitoa mhanga kuolewa na huy shujaa, kasha kumdadisi siri zake zote na kuwaambia watu wa nyumbani kwao jinsi ya kuweza kumuua, na kweli walifanikiwa kumuua kwa kushambulia kivuli chake.

Dhambi ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adamu na Eva ilisababishwa na udhaifu wa mwanamke ambae ni HAWA (EVA) kukubali kula tunda walilokuwa wamekatazawa kulila na mwenyezi Mungu. Hicho ndicho kilimfanya Adamu awe kwenye wakati mgumu sana wa kujibu maswali toka kwa Mungu hadi akaanza kujikanyaga kwa kuukwepa ukweli na kumrushia mkewe kuwa “mke uliyenipa ndiye kaniletea hilo tunda” na ndipo tukalaaniwa na sisi ambao hatujashiliki kulila hilo tunda na hatujui linafananaje.

Je, ni wangapi wanaopoteza mwelekeo wa maisha kwa sababu ya mwanamke? Je, ni mambo mangapi yameharibika hapa duniani kwa kusababishwa na mwanamke? Ni mengi na hayana maelezo mafupi. Kwa sababu hata kuenea kwa ukimwi kunasababishwa hasa na watoto wa kike kwa kuvaa nguo zenye kuleta matamanio yaani ziko fupi sana na zenye kubana maumbile kupita kipimo.

Mwisho msomaji napenda nikuambie kuwa, ukikuta serikali yoyote imeegemea sana kuwapa nafasi za juu wanawake ujue ni serikali ya kifisadi na maamuzi yake huwa yanategemea sana mwamke nyumbani kasema nini. Ni serikali yenye viomgozi ambao ni mbilikimo wa fikra za kulipeleka Taifa pazuri. Ni serikali yenye kuingia mikataba mibovu na yenye kusimama kusimamia kesi na kuishia kushindwa huku ikihukumiwa kulipa mabilioni ya fedha. Ni serikali ya watu masikini wa akili wasioweza kufanya mambo yao wenyewe bila kuomba misaada. Serikali za aina hizi ni za nchi za Afrika.

Friday, December 3, 2010

UKAME MKALI WAJA TANZANIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 10


WATANZANIA WAMEMWACHA MUNGU, WAMEELEKEA MIUNGU YA DUNIA HII.

Kama BWANA MUNGU wa Islael, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua katika Nchi hii kwa kipindi cha miaka kumi (10), ila kwa neno langu.

Bwana wa majeshi aliyezifanya mbingu na nchi kwa uweza wake mkuu na kwa mkono wake ulionyooshwa amegadhibika kwa sababu ya watu kuabudu miungu ingawa wanadai wanamjua Mungu (WAMEOKOKA) na mbaya zaidi wengine wanajiita ni watumishi wa mungu na mitume na manabii lakini kumbe ni waongo, na watu wengi wamewakimbilia watushi hao ili kutafuta mahitaji yao na si kumtafuta Mungu aliye hai. Watu wamekwenda kwa waganga wa kienyeji na wachawi kutafuta msaada badala ya kwenda kwa BWANA wa Majeshi aliyezifanya Mbingu na Nchi (wamekwenda kwa Ashuru) Hosea 5: 8-14.

Ingawa watu wanasema wanampenda BWANA, lakini ni wanafiki kabisa, ni:- Washerati, wachafu, mafisadi, waabudu sanamu, wachawi, wana uadui, wagomvi, wana wivu, wana hasira, ni watu wa fitina, ni watu wa faraka, wazushi, wanahusuda, walevi, walafi, na mambo mengi yanayofanana na hayo.

Bwana amegadhibishwa nayo, wamesikia habari za MUNGU wa kweli, lakini hawataki kumwabudu yeye. Hivyo waTanzania watashuhudia Dhiki ya Njaa kali sana ambayo haijawahi kutokea katika taifa hili. Labda katika taabu yao watatubu! Hosea 5:15.

Mungu amelijilia taifa la Tanzania kwa ghadhabu labda litatubu, na lisipotubu litaangamia.

SAMSON MLATA KUINULIWA
Mawasiliano:
+255 765 274587
+255 658 274587

SABABU 7 ZILIZOPELEKEA MAJIMBO YA NYAMAGANA & ILEMELA JIJINI MWANZA KWENDA CHADEMA KTK NGAZI YA UBUNGE NA MADIWANI.

Na: Mwandishi wetu.
Inafahamika wazi katika jimbo la Nyamagana kuwa kiongozi wa siasa hasa Mbunge kukaa madarakani zaidi ya miaka mitano ni kazi sawa na Mende kuangusha kabati au sisimizi kumeza chungwa.

Kipindi hiki matokeo yametisha sana kwa majimbo yote ya jiji la Mwanza, tumeshuhudia Magu mjini watu wakipigwa mabomu ya machozi hasa wale waliokuwa wameamua kukaa umbali wa mita 200 kusubiria hadi kieleweke, yaani kusiwepo na uchakachuzi wa kura. Vivyo hivyo mwanza mjini hasa jimbo la Nyamagana ambapo watu waliamua kuka umbali wa mita 300 na kusubiri hadi kieleweke. Chamsingi tu ifahamike wzi kuwa watu wakisema hapana na kweli huwa ni hapana, na kumwongoza binadamu ni kazi kubwa sana ambayo ni bora upewe Ng’ombe kuchunga maana utawapeleka utakako hata kwa fimbo.

Baadhi ya hisia zangu kuhusu chama cha mapiduzi (CCM) kushindwa kwa kishindo katika majimbo ya Ilemela na Nyamagana ni kama zifuatazo.

i. Watu wametapeliwa pakubwa sana na wafanya bishara ya upatu yaani DECI. Hivyo watu nadhani wamekaa na kufikiria kuwa hawa watu walikuwa na vibari kutoka seriaklini sasa je, iweje waendeshe biashara haramu namna hii bila uongozi kulitambua hilo na ukizingatia wadhili wa mambo ya ndani anaishi eneo hilihili na pia ofisi za DECI zilikuwa karibu mno na ofisi za TRA je, serikali haina vyanzo vya habari vinavyofanya kazi kwa wakati mwafaka au? tatizo liko wapi. Je, wabunge waliowapatia dhaman ya kuwasemea Bungeni walilichukuliaje hilo tatizo? Kwahiy basi kutokuonyesha mchango chanya wabunge wao kwa wananchi katika matatizo yaliyowakabili hasa DECI kumefanya wabunge hawa wamwagwe chini kuonyesha fundisho.
ii. Shirika jingine ambalo hadi sasa wanamwanza wanaliona ni la wizi ni People’s Unity for Development in Africa (PUFDIA). Wengi wametapeliwa pesan nyingi sana na mbaya zaidi walioibiwa ni wale maskini wa kutupwa, wamepewa ahadi feki, siku zimeenda hakuna matekelezo na ofisi zimefungwa hakuna hata mtu anayeonekana kuifungua hiyo ofisi. Zoezi la kukusanya pesa kutoka kwa wananchi masikini lilifanyika katikati ya jiji la Mwanza na Dar es salaam, lakini hadi sasa hakuna aliyeona mtu akinufaika na PUFDIA hivyo watu wakaamua kuinyima CCM kura katika majimbo ya Ilelema na Nyamagan.
iii. Usaliti kutoka ndani ya CCM. Inawezekana kabisa kuwa ushindi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Ilemela ukawa umesababishwa na Mbunge wa CCM jimbo la Nyamagana na pasipokujua au kwa kudhamilia kabisa mbunge wa CCM jimbo la Ilemela kukisaidia pia chama cha CHADEMA kumngo’a mbunge wa Nyamagana CCM. Haikuwa rahisi kwa mbunge wa Ilemela kuondoka madarkani kiurahisi hivi, ila tunamshukuru sana kaonyesha ukomavu wa kisiasa kwamaana alisaini mapema sana na watu hawkumwaga damu kwa kudai haki yao. Pia haijapata kutokea hapa nchini waziri wa mambo ya ndani kushindwa kwa urahisi namna hii.
iv. Machinga na mama ntilie wa jiji la mwanza wamechoshwa na wagambo kuwatimua katika maeneo yao ya kazi, awamu hii walikuwa wameamua kujiandikisha kwa wingi na kusimamia kwa asilimia zote, waliamua kuzuia njia ili yasiingie wala kutoka magari katika eneo lakujumlishia kura ili hadi kieleweke. Na kweli kilieleweka japo watu walifukuzwa sana kwa mabomu ya machozi, walichoma matairi barabarani ili hai yao ipatikane. Na mara baada ya kutangaziwa matokeo yao fujo zikatulia kabia, kumbe inapotokea njia zote za kuelekea kwenye haki zinapokuwa zimefungwa, machafuko huwa hayakwepeki. Mwanza pasingekuwa kama palivyo sasa endapo matokeo ya uchaguzi yangechakachuliwa, kwa sababu dalili zilikuwa zimeanza kuonekana mapema sana hasa kwa barabara kufungwa na raia na kuruhusu magari ya askari tu na maji ya kuwaha kupita huku wakiimba “gari letu eeh, gari letu eeh”.
v. Wananchi wamechoshwa na chama tawala, inawezekana kabisa kuwa miaka iliyopita walidanganywa kwa ahadi walizopewa hivyo wameamua kuonyesha kuwa mwaka 2010 hawadanganyiki.
vi. Aliyekuwa mgombea ubunge ambaye sasa ni Mbunge wa CHADEMA jimbo la Nyamagana Mheshimiwa WENJE kuwekewa pingamizi kuwa siyo raia wa Tanzania alijizolea umaarufu kwa watu zaidi ya mbunge wa kigoma kaskazini bwana Zitto Kabwe (CHADEMA) kipindi alifukuzwa bungeni kwa kuibua hoja nzito za ufisadi. Wananchi hasa wapiga kura wa Nyamagana waliamua kufanya mbaya dhidi ya bwana L. Masha kwa mantiki ya kuwa anatumia madaraka vibaya.
vii. Kitabu cha “Mafisadi wa Elimu” kilichoandikwa na Bwana Msemakweli kilimshushia heshima aliyekuwa mbunge wa Ilemela. Sijasema kweli yeye ni fisadi wa elimu ila naonyesha kuwa wananchi walizinduka usingizini na kuanza kufuatilia nyenendo zake kwa ukaribu zaidi.

Naomba kuishia hapa, maana hapo ndipo mwisho wa uoni wangu kuhusiana na siasa. Na mtu yeyote asije kuninukuu popote kwa sababu hizi na hisia tu “hypothesis” hazina utafiti wa kutosha. Shukrani zimwendee aliyeachia madaraka jimbo la Ilemela maana aliwahi kusaini bila bugudha yoyote ile na kwakuwa ni mjasiliamali mzuri sana basi Mwenyezi Mungu atamsaidia kukaa chini aone kakosea wapi na mara nyingine afaulu zaidi ya sasa ambapo kura hazikutosha.

Shukrani ziwaendee maaskari wote jiji la Mwanza, maana walionyesha ujasiri mkubwa sana wakati wa uchaguzi katika kuwatuliza wananchi wasifanye fujo, tena walifanikisha hilo kwa asilimia kubwa sana bila watu kumwaga damu.

Mwisho liwe fundisho kwa wote wenye nia ya kuongoza wananchi maana hata ninyi mliokamata nafasi hizo sasa hivi uchaguzi ijao mnaweza kung’atuliwa kwa ulaini sana endapo mtabolonga bungeni. Hatujawatuma mkasinzie mjengoni, tumetuma wawakilishi wenye kutoa hoja kwa mujibu wa sheria na vifungu, wenyekuvumilia vitisho kutoka vyama pinzani na kuongea vitu mlovifanyia utafiti wa kutosha huku mkikumbuka kuwa mnaongoza wananchi waliokaliwa na mataifa ya kibepari yaliyorudi tena kwa gia ya uwekezaji “full exploitation”. Piganieni kuibadili katiba ya nchi, na kutengua mikataba mibovu na kuchunguza makampuni yanayobadili majina kama CELTEL-ZAIN-AIRTEL TZ. Chunguzeni kuna ukweli wowote hapo au ni wizi mtupu, kupitia ukwepaji kodi serikalini. Mungu ibariki Tanzania.

+255 783 700083