Thursday, June 3, 2010

SAUT YAINGIA MGOGORO NA RITA

Taasisi, asasi 200 kufutwa nchini

Thursday, 03 June 2010 09:05
Na Boniface Meena

http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/2136-taasisi-asasi-200-kufutwa-nchini

OFISI YA kabidhi wasihi nchini, Rita, imetoa notisi ya kusudio la kufuta taasisi 200 nchini, yakiwamo makanisa, misikiti na vyuo vya elimu ya juu.

Rita imetoa notisi hiyo jana ikieleza kwamba sababu za kuchukua hatua hiyo ni taasisi hizo kushindwa kutekeleza majukumu na wajibu wao kwa mujibu wa sheria.
Kaimu msimamizi mkuu wa Rita, Phillip Saliboko ametaja katika notisi hiyo kuwa miongoni mwa vyuo vya elimu ya juu vitakavyoathirika ni Chuo Kikuu cha St.Augustino kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki pamoja na misikiti miwili ya dini ya Kiislamu jijini Dar es Salaam.

Katika maelezo hayo, Rita imeeleza kuwa imepewa mamlaka hayo na sheria, ikitaja sura ya 318 ya toleo la mwaka 2002, kifungu cha 23(1)(d) ambayo inamruhusu wakala huyo kuzifuta asasi ambazo zimeshindwa kutekeleza majukumu na wajibu wao.

Taasisi na asasi zilizotajwa ni pamoja na vyuo vya elimu ya juu nchini, shule za msingi, makanisa pamoja na asasi zisizo za serikali (NGO).

Notisi hiyo inaeleza kuwa moja ya sababu za kuzifuta asasi hizo ni kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko katika asasi hizo na kutokufanya marejesho ya wadhamini kwa kipindi kirefu baada ya usajili.

"Kwa hiyo ninatoa taarifa kwamba ninakusudia kufuta udhamini wa asasi hizo baada ya kwisha kwa kipindi cha siku 30 baada ya tarehe ya notisi hii.

Labda kama kutakuwapo na sababu zozote za msingi na za kisheria zitakazoniridhisha kwa nini nisifute udhamini wa asasi hizo,"anaeleza Saliboko katika taarifa yake.

Baadhi ya makanisa ambayo yametajwa kwenye notisi hiyo ni Kanisa la Anglican Sumbawanga, Kanisa la Pentekoste Korogwe, Morogoro na Iduguta.

Misikiti ni pamoja na msikiti wa Masjid Ghalib Islamic Centre na Masjid Qadiria ulio Mbagala Charambe na Mianzini Temeke jijini Dar es Salaam.

Taasisi nyingi zilizotajwa ni za maendeleo, vituo vya kulea watoto yatima na nyingi zipo jijini la Dar es Salaam.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

No comments:

Post a Comment